Kwa Yesu hakuna kulia
Hakuna kujuta
Hakuna Huzuni

Kwa Yesu kuna Furaha
Kuna Amani
Kuna kila kitu

Ninapaswa kutulia kwa Bwana
Sijui wewe
Ukristo wa kweli ni “namna ya kuishi.” Yesu alinena kwa dhairi kabisa katika Luka 4:4, “Binadamu hataishi kwa mkate pekee, bali kwa kila neno la Mungu.” (Luka 4:4). Biblia sio tu ni mwongozo wa imani yetu ya kila siku; ni neno la Mungu, linaloonyesha jinsi ya   
kuishi ndani ya Mungu, namna ya kupenda, kutoa, na kumtumikia. Kristo anatufundishakuishi katika hivyo.  Pia, Biblia ni msingi wa elimu ya kweli. Yesu alisema, “…Mtaujua ukweli, nao ukweli utawapeni uhuru” (Yohana 8:32).
  
Utengano huu unamaanisha kwamba wale ambao Mungu amewaita watishi maisha tofauti na wale waliokaribu nao, na kwa namna ya kwel “mabalozi” wa serikali ya Mungu. (Waefeso 6:20; 1 Petro 2:9-10). Wakristo wanapaswa kuwaombea viongozi wa mataifa yao, ambao Mungu amewaweka hapo, lakini katika historia Kanisa la Mungu linafunza washirika wake wasishiriki katika siasa za dunia.
Uponyeshaji mtakatifu ni moja wapo ya manufaa ya kuishi ndani ya Mungu. Uponyeshaji ni moja wapo ya “zawadi za kiroho” (1 Wakorintho 12:1,9). Mojawapo ya Jina la Mungu la Kihibrania ni Yahweh Ropheka, likimaanisha “Mwenye Enzi anayeponya”. Mungu ni Mwenyezi Mkuu anaye “samehe dhambi zako zote, anaeponya magonjwa yako yote” (Zaburi 103:3; 1 Petro 2:24). “Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.
Basi, ungamanianeni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.” (Yakobo 5:14-16).
 
Kanisa Hai la Mungu linafuata maagizo haya ya moja kwa moja ya bibilia. Tunaamini kwamba Mungu anaponya sasa kulingana na imani ya mtu na mapenzi ya Mungu katika kila jambo. 
Neno la Mungu linaamuru binadamu wote wapende majirani zao kama wanavyo jipenda wenyewe (Walawi 19:18; Mathayo 22:39; Mitendo ya Mitume 17:24-29). Mungu anafunua kwamba wokovu unatolewa wazi kwa Wayahudi na Wasio wayahudi  (Matendo ya Mitume  10:34-35; Warumi 10:12-13; cf. Yoeli 2:32). Tunaamini kwamba upendo na heshima unapashwa uonyeshwe kwa watu wa makabila yote (Warumi 13:10).
            Kujua zaidi juu ya namna maisha ndani ya Mungu yanavyoweza kukuletea amani kuu na 
            mafanikio, soma kijitabu chetu, Amri Kumi. 





Nazidi kubarikiwa na likizo yangu ,,,,Barikiwe pia mama uliye mleta Neema Mbise Duniani....nami nasimamia katika kitabu cha Nabii Yeremia 1;10


Watu wengi wanatafuta “hatua kuelekea wokovu.” Watu wanapenda dhana ya kitabu cha mwongozo wa hatua tano, kwamba ikiwa sitafuatwa, zitaelekeza wokovuni. Mfano wa haya ni Waislamu na nguzo zao tano. Kulingana na Waislamu, ikiwa nguzo hizo tano zimefuatwa wokovu utapatikana. Kwa sababu ya dhana ya mchakato wa hatua kwa hatua kwa wokovu ni wa kusihi, wengi wa Wakristo katika jamii wanawazilisha wokovu kuwa kama ni ule upatikanao kwa ajili ya kufuata mchakato wa hatua kwa hatua. Kinisa la Kikatholiki la Kirumi liko na sakaramenti saba. Madhehebu mbali mbali la Wakristo wanaongeza ubatizo, kutubu hadharani, kugeuka kutoka dhabi na kuongea katika ndimi na kadhalika, kama hatua za wokovu. Lakini Biblia yawazilisha hatua moja ya wokovu. Wakati mfilipi mfungwa alimwuliza Paulo, “Nitafanya nini ili niokoke?” Paulo alimjibu, “Mwamini Bwana Yesu na utaokolewa” (Matendo 16:30-31)

Imani katika Yesu kama mwokozi ndio “hatua” pekee ya wokovu. Ujumbe wa Biblia uu wazi. Wote tumetenda dhambi kinyume na Mungu (Warumi 3:23). Kwa sababu ya dhambi zetu, tunastahili kutenganishwa na Mungu milele (Warumi 6:23). Kwa sababu ya upendo wake kwetu (Yohana 3:16), Mungu aliuchukua umbo la mwanadamu na akafa kwa ajili yetu, huku akichukua adhabu ambayo tulistahili (Warumi 5:8; 2Wakorintho 5:21). Mungu anaahidi msamaha wa dhambi na uzima wa milele mbinguni kwa wote wampokeao, kwa neema kupitia kwa imani katika Yesu Kristo kwa mwokozi (Yohana 1:12; 3:16; 5:24; Matendo 16:31).

Wokovu sio juu ya hatua fulani ambazo ni lazima tuzifuate ile tupate wokovu. Naam, Wakristo lazima wabatizwe. Naam, Wakristo lazima wamkiri hadharani Kristo ni mwokozi. Naam Wakristo lazima wageuke kutoka dhambi. Naam, Wakristo lazima wayatoe maisha yao kwa kumtii Mungu. Ingawa, hizi sio hatua za wokovu. Ni matokeo ya wokovu. Kwa sababu ya dhambi zetu, kwa njia yoyote hatuwezi jipatia wokovu. Tunaweza fuata hatua 1000, na hazitatosha. Ndio sababu Yesu akafa kwa ajili yetu. Kamwe hatuna uwezo wa kulipia dhambi zetu kwa Mungu kama deni ili tujitakaze kutoka dhambi. Ni mungu pekee angekamilisha wokovu, na kwa hivyo alifanya. Mungu mwenyewe alikamilisha “hatua” na papo hapo akautoa wokovu kwa ye yote atakayeupokea kutoka kwake.

Wokovu na msamaha wa dhambi sio mambo na hatua. Ni kumpokea Kristo kama mwokozi na kutambua ya kwamba amekwisha fanya kazi yote kwa niapa yetu. Mungu anahitaji hatua moja kutoka kwetu-kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi na kumwamini Yeye pekee kama njia ya wokovu. Hiyo ndio yatofautisha imani ya Kikristo kutoka kwa dini zote za ulimwengu, ambazo kila moja iko na orodha ya hatua ambazo ni lazima zifuatwe ili wokovu upatikane. Imani ya Kikristo yatambua ya kwamba Mungu amekwisha kamilisha hatua, na anatuita tumpokee kwa imani.
Biblia inazungumzia juu ya vitu hivi tulivyonavyo ili tushinde maisha yetu ya dhambi:

(1) Roho Mtakatifu – kipawa kimojachapo ambacho Mungu ametupa (kanisa lake) kwa ajili ya kuwa na ushindi katika maisha ya kikristo ndani ya Roho Mtakatifu. Mungu anatofautisha mtendo ya mwili na matunda ya Roho Mtakatifu katika wagalatia 5:16-25. katika andiko hilo tunashauriwa kutembea katika uwepo wa Roho Mtakatifu. “waumini wote tayari wamejazwa na Roho Mtakatifu”,lakini hapa tunasisitizwa kupatia nafasi Roho Mtakatifu atutawale na kutuongoza. Hii ina maana ya kuwa tusikilize sauti yake tusije tukatenda mapenzi yetu wenyewe.

Tofauti ambayo Roho Mtakatifu anaweza kuifanya maishani mwa mtu ni kama ile ya Petro, kabla hajajazwa Roho Mtakatifu alimkana Yesu mara tatu, na alikuwa mbeleni ameahidi kumfuata Yesu mpaka kwenye hatari ya kifo angekufa naye. Baada ya kujazwa na Roho alizungumza waziwazi na kwa ujasiri mbele ya wayahudi juu ya mwokozi katika siku ya pentekote.

Unatembea ndani ya Roho ukiwa humzuii anapotaka kujidhihirisha (“kumzima Roho” wathesalonike wa kwanza 5:19) na una kiu ya kujazwa naye kila wakati (Waefeso 5:18-21). Je mtu hujazwaje na Roho Mtakatifu? Kwanza ni kwa mapenzi ya Mungu kama vile ilivyo katika agano la kale. Alikuwa akichagua watu Fulani, kuwajaza kwa ajili ya kutekeleza kazi ama wadhifa Fulani (Mwanzo 41: 38; Kutoka 31:3; Hesabu 24:2; Samueli wa kwanza 10:10; na kadhalika.) Ninaamini kuwa kuna ushahidi katika Waefeso 5:18-21 na Wakolosai 3:16 yakuwa Mungu huchagua kujaza wale wanaojijaza Neno la Mungu kwa kuwa kote kote ni kujazwa uwezo wa Mungu.

(2) Neno la Mungu, Biblia – Timotheo wa pili 3:16-17 inasema ya kwamba Mungu ametupa neno lake ili lituandae katika kufanya kazi njema. Linatufundisha jinsi ya kuishi na cha kuamini, linatufunulia kama tumetenda makosa na kuturudisha katika njia ya sawa. Kama waebrania 4:12 inavyosema Neno la Mungu liko hai na lina nguvu ya kupenya ndani ya nafsi zetu kung’oa lile tatizo ambalo mwanadamu hangeweza kulitatua. Mwandishi wa zaburi azungumzia uwezo wa Neno la Mungu juu ya kubadilisha maisha ya watu katika zaburi 119:9,11,105 na aya nyengine. Joshua aliambiwa siri ya kushinda adui zake (inayoashiria pia vita vyetu vya kiroho) ni kwamba asilisahau Neno la Mungu bali alitafakari usiku na mchana ili akalitimize. Haya aliyatenda, ijapokuwa maagizo yenyewe hayakuwa na uhusiano na mambo ya kivita lakini yakampa ushindi katika vita vya kuimiliki nchi ya ahadi.

Hii ni sehemu ambayo mara nyingi tunaipuuza. Tunapenda kubeba biblia tukienda kanisani ama kusoma aya za kukariri lakini hatuyatilii maanani yale tuyasomayo. Hatuyatafutii nafasi maishani mwetu kiasi cha kutubu dhambi zetu na kumtukuza Mungu kwa kipawa hiki. Tunasoma tu kiasi cha kupata mtazamo Fulani juu ya wokovu lakini hatuongezi juhudi zozote katika kutafakari kwetu mara kwa mara kiasi cha kutufanya tuwe na afya nzuri kiroho.

Ni muhimu sana kwako ufanye tabia ya kusoma neno la Mungu. Kama bado hujazoea basi Roho anakusisitiza uwe na tabia ya kulisoma Neno la Mungu. Nina kushauri uwe na kumbukumbu ya yale uliyoyasoma kwa kuyanakili kwenye daftari lako au kwenye kompyuta. Biblia ndicho kifaa Roho hutumia katika maisha yetu na maisha yaw engine (Waefeso 6:17), ikiwa ni sehemu kubwa ya silaha mojawapo ambayo Mungu hutupa ili tupigane vita vya kiroho (Waefeso 6:12-18)!

(3) Maombi – Hii pia ni njia nyengine ambayo Mungu ametupatia. Njia hii wakristo wengi huitaja tu kwa maneno lakini hawaitumii. Tuna ibada za maombi na nyakati za maombi na kadhalika lakini hatuoni manufaa ya jambo hilo sawa na kanisa la kwanza (Matendo 3:1; 4:31; 6:4; 13:1-3, na kadhalika). Paulo mara kwa mara arudia kueleza vile alikuwa akiwaombea wale aliokuwa akiwahudumia. Lakini tunapokuwa peke yetu hatuitumii njiaa hii. Mungu ametuahidi mambo mazuri ya ajabu kuhusiana na maombi (Mathayo 7:7-11; Luka 18:1-8; Yohana 6:23-27; Yohana wa kwanza 5:14-15, na kadhalika.) Paulo analiongezea mkazo tena katika mafundisho yake juu ya kujiandaa kwa ajili ya vita vya kiroho (Waefeso 6:18)!

Je, ni muhimu kiasi gani njia hii? Tunapomtazama tena Petro, tunaona maneno ya kristo aliyomwambia kabla hajamkana kule Gethsemane. Yesu alipokuwa akiomba Petro alilala. Yesu akamwambia, “Kesheni mkiomba ili msiingie majaribuni: Roho inataka lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:41). Wewe pia kama Petro unataka kufanya mema lakini huna nguvu yakutosha kufanyia hayo. Lazima tufuate mausia ya Mungu, tuendelee kumtafuta, tukibisha na kumuuliza… na atatupatia nguvu ile tuitafutayo (Mathayo 7:7 na kuendelea). Lakini lazima tuitilie mkazo njia hii maishani mwetu ndiyo tufaulu. Sisemi ya kwamba maombi ndiyo njia maalum zaidi. La sivyo. Mungu ni wakutisha. Maombi ni kukubali hali zetu za udhaifu, ukuu wa Mungu mwenye nguvu na asiyeshindwa ili tupate uwezo huo huo tuweze kuyafanya yaliyo mapenzi yake (wala si yetu) (Yohana wa kwanza 5:14-15).

(4) Kanisa – Hii ni mojawapo ya njia tunazozifumbia jicho. Yesu alipowatuma wanafunzi wake aliwatuma wawili wawili (Mathayo 10:1). Tunaposoma juu ya habari za safari za wale wamishenari katika kitabu cha matendo ya mitume, hawakuenda mmoja mmoja bali katika makundi, wawili wawili au zaidi.Yesu alisema mahali wawili au watatu wamekusanyika kwa ajili ya jina langu, nami nitakuwa katikati yao (Mathayo 18:20). Anatuamuru tusiache kukusanyana pamoja kama kawaida za watu wengine zilivyo bali tuutumie wakati wa kuwa pamoja kwetu kwa kutiana moyo katika upendo na matendo mema (Waebrania 110:24-25). Anatuagiza kutubu dhambi zetu mmoja kwa mwingine (Yakobo 5:16). Katika habari za hekima katika agano la kale tunaambiwa ya kwamba chuma hunoa chuma mwenziwe, vivyo hivyo mtu huchangamsha sura ya rafiki yake (Methali 27:17) “kamba ya nyuzi tatu haikatiki rahisi.” “kuna nguvu katika umoja wa wengi (Mhubiri 4:11-12).

Baadhi ya watu ninaowafahamu wamepata kaka na dada katika kristo wanaotangamana pamoja au kwa simu na wanaelezana vile wanaendelea na maisha ndani ya kristo na wanawajibika katika kuombeana huku wakiishi maisha sawa na Neno la Mungu. Mabadiliko mara nyingine huja haraka na wakati mwengine polepole. Lakini Mungu ametuahidi ya kwamba kadri tunavyoendelea kutumia njia hizi alizotuwekea, ndivyo atatuletea mabadiliko maishani mwetu. Vumilia ukijua ya kuwa ni mwaminifu katika ahadi zake.

Wakorintho wa kwanza 15: 1-4 inasema, “Tena ndugu zangu, ninawatangazia tena ile injili ambayo nimekwisha kuwahubiri ambayo mmeipokea nakusimama ndani yake; ambayo kupitia hiyo mmeokolewa mkiendelea kukumbuka yale niliyowahubiri msije mkawa mmeamini bure. Kwa kuwa niliwapatia kwanza kile nilichokuwa nami nimepokea, kwa jinsi ile Yesu aliyokufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na maandiko; na akazikwa, hatimaye akafufuka tena siku ya tatu kulingana na maandiko.

Kwa kifupi hii ndiyo imani ya kikristo. Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya mkristo ya Roho Mtakatifu.

Wakristo huamini ya kuwa biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.

Wakristo huamini yakwamba mwanadamu aliumbwa ili awe na ushirika na Mungu lakini dhambi hutenganisha watu wote na Mungu (Warumi 5:12, Warumi 3:23). Imani ya kikristo hufundisha ya kwamba Yesu kristo alitembea juu ya ardhi akiwa Mungu kamili na huku akiwa pia mwanadamu (Wafilipi 2:6-11), na akafa msalabani. Wakristo huamini ya kwamba, baada ya kifo chake msalabani, Yesu alizikwa, akafufuka na sasa anakaa upande wa kuume wa Mungu Baba akiwaombea waumini milele (Waebrania 7:25). Imani ya kikristo inasema ya kwamba kifo chake Yesu kristo msalabani kilitosha kufidia dhambi za watu wote na hili ndilo linalorejeza ushirika baina ya Mungu na mwanadamu (Waebrania 9:11-14, Waebrania 10;10, Warumi 6:23, Warumi 5:8).

Ili uokolewe, sharti uweke imani yako juu ya kazi Yesu aliyoimaliza msalabani. Mtu akiamini kuwa Yesu alikufa mahali pa yeye ili amlipie gharama zake za dhambi na akafufuka tena basi mtu huyo ameokoka. Hakuna kitu mtu anachoweza kufanya mwenyewe binafsi ili aokoke. Hakun mwema wa kutosha kumpendeza Mungu kwa kuwa sote ni wenye dhambi (Isaya 64:6-7, Isaya 53:6). Lengine ni kwamba hakuna cha ziada maana kazi yote ilifanywa na kristo! Alipokuwa msalabani, Yesu alisema, “Imekwisha” (Yohana 19:30).

Kama vile haikugharimu chochote kuokolewa ila kuamini kazi iliyofanywa na Yesu msalabani vile vile hakuna kazi ambayo unahitajika kufanya ili upoteze wokovu wako. Kumbuka kazi ilifanywa na kumalizwa na yesu! Hakuna chochote kinachotegemea wewe mwenyewe katika wokovu. Yohana 10:27-29 inasema “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na ninawajua na wao hunifuata. Nami huwapa uzima wa milele; nao hawatapotea wala hakuna awezaye kuninyang’anya kutoka mikononi mwangu. Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa kutoka mikononi mwa Baba.”

Wengine hufikiria nakusema, “Nikiokolewa tu naweza kufanya kila nitakacho na wala sitapoteza wokovu wangu!” lakini wokovu si juu ya kuwa huru kufanya mapenzi yako. Wokovu ni kuwa huru kutoka kwa nyororo za dhambi ulizokuwa ukizitumikia iliuwe huru kumtumikia Mungu. Kadri waumini wanavyoishi duniani, kutakuweko na hali ya kupingana na dhambi katika miili yao. Kuishi na dhambi kunazuia ushirika na Mungu na muumini yeyote atakaye amua kuishi na dhambi hatafurahia ushirika wake na Mungu. Hata hivyo wakristo wanaweza kushinda dhambi kwa kulisoma na kulitumia neno la Mungu (biblia) maishani mwao na kuongozwa na Roho Mtakatifu – hiyo ina maana ya kujiachilia uongozwe na Roho katika kila shughuli ya siku na pia kupitia Roho uheshimu neno la Mungu.

Kwa hivyo, huku dini nyingine zikitaka waumini wao watende mambo Fulani Fulani au wasitende mambo Fulani ukristo ni juu ya kuwa na ushirika na Mungu. Deni lako la dhambi limelipwa na unaweza kuwa na ushirika na Mungu. Unaweza kuwa na ushindi juu ya maisha yako ya dhambi na ukatembea na ushirika na Mungu ukiwa mtiifu. Huwo ndiwo ukristo wa kweli unaoelezewa katika Biblia.
Je, kuna Mungu? Ninaona ni jambo la kusisimua ya kwamba umakini mwingi umepawa mjadala huu. Katika takwimu zetu hivi sasa zasema ya kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watu duniani wanaamimi kuweko kwa Mungu au Mamlaka ya kiwango cha juu. Jukumu linabaki kwa wenye kuamini kuthibitisha ukweli wa kuweko kwake. Mimi nafikiri ingewapasa wale hawaamini watuthibitishie.

Kuweko kwa Mungu hakuwezi kutothibitishwa wala kuthibitishwa. Bibilia inasema inatupasa kukubali kwa imani kuwa Mungu yuko, “Na pasipo imani haiwezekani mtu kumpendeza Mungu, kwa kuwa kila ajaye kwake sharti aamini kuwa yuko na ya kuwa huwapa vitu wale wamtafutao kwa bidii” (Waebrania 11:6). Kama Mungu alingetaka iwe, angejitokeza tu mbele ya ulimwengu wote kuwajulisha wote kuwa yeye yuko. Lakini, angefanya hivyo hakungekuwa na haja ya imani. “Tena Yesu kamwambia, ‘kwa kuwa umeniona, umeamini; heri wale ambao hawakuniona na wameamini” (Yohana 20:29).

Hiyo haimaanishi ya kuwa hakuna idhibati ya kuweko kwa Mungu. Biblia inasema, “Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu; anga zatangaza kazi za mikono yake. Siku baada ya siku zamimina hotuba zake; usiku baada ya usiku zaonyesha ufahamu. Hakuna hotuba au lugha ambayo haisikiki. Sauti zao hutapakaa duniani kote, maneno yao mpaka mwisho wa dunia” (Zaburi 19:1-4). Ukitazama nyota, ukijaribu kufahamu kina cha anga, na kutazama maajabu ya kiasili, huku ukiona urembo wa kutua kwa jua - haya yote yanaashiria kuweko kwa Mungu muumbaji. Kuna ushahidi wakuweko kwa Mungu ndani ya mioyo yetu. Mhubiri 3:11 inatuambia, “….ameweka pia umilele ndani ya mioyo ya wanadamu…” Kuna kitu ndani yetu kinachotujulisha ya kuwa kuna kitu zaidi baada ya maisha haya tunayoishi na mwingine zaidi yetu nje ya dunia hii. Hata tukipuuza bado kuna uwepo wa Mungu maishani mwetu. Biblia inatuonya ya kuwa kuna wengine watakuwapo watakaokataa kuwepo kwa Mungu, “Mjinga amesema moyoni mwake hakuna Mungu” (Zaburi 14:1). Kwa kuwa zaidi ya asilimia 98 ya watu wa tamaduni mbali mbali katika vizazi vilivyopita ndani ya mabara yote duniani ni waumini wa kuwepo kwa Mungu wa aina Fulani – lazima kuwe kuna mtu ama kitu Fulani kinachohisi na kusababisha imani hii.

Kuongezea, kuna maoni mbali mbali ambayo hutumika kuthibitishia pia. Maoni ya kwanza yasema kwa kuwa Mungu ni kile ambacho zaidi yake hakuna. Basi uwezekano wa kuwepo kwake ni mwingi. Na kama Mungu hayuko basi hakungekuwa na ambacho zaidi yake hakuna. Maoni ya pili ni kwamba kwa kuwa ulimwengu unaonyesha kazi nzuri ya ustadi iliyofanyika basi lazima kuweko na aliyeifanya. Kila kitu kina fanya kazi vyema kwa wakati wake na kwa kipimo mwafaka. Kama hewa yetu ingeharibika tu kidogo viumbe vyote vingekufa.

Maoni ya tatu ni kwamba kwa chochote kufanyika lazima kuweko na mwenye au chenye kusababisha. Kwa vile ulimwengu upo lazima kuwe na aliyeusababisha uweko na huyo ndiye Mungu. Maoni ya nne ni kwamba katika kila utamaduni, mila na desturi za watu duniani kuna aina Fulani ya mfumo wa sheria ya kuelekeza; yenye kutambua mema na mabaya. Kuua, uongo, wizi na uchafu wa kitabia ni mambo yanayokataliwa ulimwenguni kote. Hali hii ya kutambua meme na mabaya ilitoka wapi Kama si kwa Mungu Mtakatifu?

Biblia inatuambia, watu watakataa ukweli wa kuweko kwa Mungu na kuamini roho za uongo. Warumi 1:25 inasema, “walibadilisha ukweli wa Mungu na kutumikia uongo hata kuiabudu na kuitumikia miungu waliyoiumba kwa mikono yao kinyume na Mungu aliyewaumba –ambaye daima husifiwa. Amina.” Biblia pia inasema, watu hawana sababu ya kutomwamini Mungu, “Kwa kuwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu siri za uwepo wake – Nguvu zake za milele na utisho wake umethibitika na kufahamika kutokana na yale aliyoyatenda kwa hivyo wanadamu hawana kisingizio” (Warumi 1:20).

Watu husema hawamwamini mungu kwa sababu si kisayansi ama hakuna kithibitisho cha kuweko kwake. Sababu halisi ni kwamba kwa kukubali yuko,mtu anahitajika kuwajibika mbele zake na kuomba msamaha (Warumi 3:23; 6:23). Kama Mungu yuko basi tunawajibika kwa matendo yetu. Kama hayuko, basi tunaweza kufanya mapenzi yetu wenyewe bila kujali hukumu. Huenda ikawa hii ndiyo sababu ya watu wengine kushikilia mawazo ya kuwa dunia ilifanyika tu kwa njia ya vitu tofauti tofauti kubadilika umbo polepole kupitia mabadiliko ya kimazingira ili waepukane na ukweli wa kuna Mungu muumbaji wa yote. Mungu yuko na kila mmoja anajua hivyo. Mwenye kubishana ni mbishani tu lakini huwa hata yeye anajua yuko.

Je, nitajuaje kuwa Mungu yuko? Najua Mungu yuko kwa kuwa nazungumza naye kila siku. Simsikii masikioni akinijibu lakini ninahisi uwepo wake, nahisi kuongoza kwake, najua upendo wake ninatamani neema yake.Mambo yaliyotendeka maishani mwangu hayana maelezo mengine ila Mungu. Mungu ameniokoa kimiujiza na kuyabadilisha maisha yangu mpaka sasa nimebaki tu kumtukuza. Maelezo haya yote hayawezi kumfanya mtu anayetaka kukataa kuwepo kwa Mungu akubali. Muhimu ni kumkubali kwa imani (Waebrania 11:6). Imani kwa Mungu si bure kama kubahatisha gizani bali ni sawa na kutembea salama ndani ya chumba chenye nuru ambamo asilimia 90 ya watu waliomo wamesimama.
Yesu kristo ni nani? Watu wachache sana huuliza kama Yesu kristo alikuweko. Inakubalika kikamilifu kuwa Yesu alikuwa ni mtu aliyetembea juu ya ardhi huko Israeli karibu miaka 2000 iliyopita. Mjadala huzuka wakati wa utambuzi kamili wa Yesu kristo unapojadiliwa. Karibu kila dini kubwa humtaja Yesu kama nabii, mwalimu mwema au mcha mungu. Tatizo ni kuwa Biblia inatuambia ya kuwa Yesu alikuwa zaidi ya nabii, mwalimu mwema au mcha mungu.

C.S. Lewis, katika kitabu chake kiitwacho ukristo wa kijinsia tu aeleza yafuatayo: “nipo hapa kuzuia yeyote asemaye upumbavu kama wengine wao juu ya Yesu kristo. Wao husema, “Niko tayari kumkubali Yesu kama mwalimu wa uadilifu tu lakini sikubali madai yake ya kuwa ni Mungu”. Hili jambo moja lapo ambalo tusiliseme. Mtu aliyekuwa mwanadamu wa kawaida na kuweza kusema yale Yesu alisema bila shaka angekuwa mwendawazimu ama ibilisi wa kuzimu. Lazima ufanye uamuzi kamili. Uamue kama Yesu alikuwa mwana wa Mungu au mwendawazimu. Unaweza kumtusi, kumtemea mate na hata kumdharau. Hakutuachia nafasi ya kumuamulia Yeye kuwa ni nani.

Je, Yesu alisema yeye ni nani? Je, biblia inatuambia alikuwa nani? Kwanza tutazame maneno ya Yesu kutoka Yohana 10:30, “Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa juu juu, hapa hakuna taswira ya kuwa yeye pia ni Mungu. Lakini ukitazama majibizano ya wayahudi dhidi ya maneno yake, “Hatukupigi mawe kwa sababu nyinginezo ila kwa hili, kukufuru. Wewe ni mwanadamu tu lakini unajifanya sawa na Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa usemi wake Yesu ulimaanisha kuwa yeye ni Mungu. Katika andiko lifuatalo Yesu hakuwasahihisha kwa kusema, “si kuleta madai ya kuwa ni Mungu.” Ina maana ya kuwa Yesu alikuwa akisema kuwa yeye ni Mungu kwa msemo huwo, “Mimi na Baba yangu ni mmoja.” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwengine. Yesu alisema, “Amini, Amini nawaambia, kabla Abraham kuweko Nilikuwako.” Hali iliyowasukuma wayahudi kushika mawe iliwampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Yesu kutangaza kitambulisho chake kama, “Mimi ndimi” ambalo ni jina lilitumika sana kumaanisha Mungu katika Agano la kale ni ishara kuwa ni Mungu (Kutoka 3:14). Kwa nini wayahudi walitaka kumpiga mawe kama hakuwa amesema kitu ambacho kwao ni kufuru, madai ya Yesu kuwa ni Mungu?

Yohana 1:1 yasema, “na Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 yasema, “ na neno akafanyika mwili”. Hii ina maana ya kuwa Yesu ni Mungu katika mwili. Tomaso, mwanafunzi wa Yesu alisema, “Bwana wangu na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi. Mtume Paulo amtaja kama, “… Mungu wetu mkuu na mwokozi Yesu kristo” (Tito 2:13). Mtume petro asema, “Mungu wetu na mwokozi Yesu kristo” (Petro wa pili 1:1). Mungu Baba ni shahidi wa kuthibitika kwa Yesu Kristo, “Na kwa ajili ya mwana asema, “Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, kitadumu milele na milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.” Unabii wa Agano la kale wamtaja Yesu kama Mungu, “Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa. Kwetu mtoto tumepawa na ufalme utakuwa mabegani mwake. Na ataitwa Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, mfalme wa amani.”

Kwa hivyo, kama C.S. Lewis alivyosema, kumtaja yesu kama mwalimu mwema tu si sawa. Yesu alikiri waziwazi kuwa yeye ni Mungu. Kama si Mungu basi ni muongo na si nabii, mwalimu mwema wala mcha mungu. Wanavyuoni wa sasa, husema, “Yesu yule wa kihistoria” hakusema mengi ya yale biblia inyomtaja nayo. Sisi ni wakina nani hata tupinge neno la Mungu kuhusu kile Yesu alisema ama kufanya? Mwanachuoni huyo wa miaka zaidi ya elfu mbili baada ya Yesu atakuwa na mtazamo gani wa kweli kushinda wale walioishi na kumtumikia Yesu kristo huku wakifundishwa pia (Yohana 14:26)?

Ni kwa nini, swali juu ya Yesu ni nani, ni muhimu? Kuna tatizo gani kama Yesu kweli ni Mungu au la? Swala muhimu linalompasa Yesu kuwa Mungu ni kwamba, kama si Mungu, kufa kwake hakungetosha kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu tu ndiye angeweza kufidia adhabu hiyo (Warumi 5:8; Wakorintho wa pili 5:21). Ilimlazimu Yesu kuwa Mungu ili alipe deni zetu. Yesu ilimbidi awe mwanadamu ili afe. Wokovu wapatikana tu kwa imani juu ya Yesu kristo! Uungu wa Yesu ndio unao sababisha yeye kuwa Njia ya pekee ya wokovu. Uungu wa Yesu ndio uliomfanya kukiri, “Mimi ndimi njia kweli na uzima. Hakuna ajaye kwa Baba ila kupitia Mimi” (Yohana 14:6).


>>>>>www.gotquestions.org

Yesu hakunakiliwa mahali popote katika biblia akisema, “Mimi ni Mungu.” Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba hakusema kuwa yeye ni Mungu. Kwa mfano ni maneno ya Yesu katika Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa kwanza, hili linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. 

Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa matamshi ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu. Katika aya zifuatazo hawasahihishi wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwingine.

 Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?

Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!

Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”

Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.

Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia dhambi za ulimwengu wote w (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti.