CHANGAMOTO KATIKA MAISHA YA UJANA
Katika maisha ya ujana kuna
changamoto mbali mbali ambazo kijana ana wajibu wa kuzishinda, basi hebu tuone
baadhi ya vijana na changamoto
walizokutana nazo;
Kijana Yususfu aliyependwa zaidi na mzee
Yakobo, alichukiwa na ndugu zake hata wakapanga kumwua kwa
kuwa alipendwa zaidi na baba yao;
“Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda
kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa
amani.”............
Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya
shauri juu yake ili wamwue. Wakasema wao kwa wao, Tazama, yule bwana ndoto
anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi
tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.” (Mwanzo
37:4, 18-20)
Kijana Yusufu alisingiziwa uovu na
mke wa Potifa hata kufungwa gerezani; “Ikawa
alipoona ya kwamba amemwachilia nguo yake mkononi mwake, naye amekimbia nje,
akawaita watu wa nyumbani-
mwake, akasema nao, akinena,
Angalieni, ametuletea mtu Mwebrania
atufanyie dhihaka. Ameingia kwangu, ili alale nami, nikalia kwa sauti kuu.
Ikawa aliposikia ya kuwa nimepaza sauti yangu na kulia, aliiacha nguo yake
kwangu,akakimbia, akatoka nje......... Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya
mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitenda mambo kama haya, hasira
yake ikawaka. Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa
wafungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani.” (Mwanzo 39:13-15, 18-20)
Katika siku za mfalme Nebukadreza,
aliam uru vijana watatu, yaani Shadraka Meshaki na Abednego kutupwa katika
tanuru la moto kwa kuwa waligoma kuiabudu sanamu. “
Basi Nebukadreza akatoa amri kwa
hasira na ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego
Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme. Nebukadreza
akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni makusudi
hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha?...............
Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao,
na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka
moto.” (Danieli 3:13-14, 21)
Kipengele: Habari mpya, Vijana
0 Maoni