Ni Dini gani ya kweli inifaayo?
Migahawa ya vyakula vya haraka hutushawishi kwa kuturuhusu kuagiza
vyakula jinsi ile tungelivitaka. Mikahawa fulani hujivunia mara mia moja
tofauti za ladha na aina za Kahawa. Hata wakati mtu anaponunua Nyumba
au Magari, hutafuta moja iliyo na mambo tofauti na ambayo ina kila kitu
ambacho angetamani. Hatuishi tena tu katika Ulimwengu wa chocolate,
Vanilla au strawberry. Chaguo ni Mfalme! Unaweza kujitafutia kitu
chochote utakacho kulingana na mapenzi yako kibinafsi au mahitaji yako.
Sasa waoneleaje kuhusu Dini ambayo itakuwa ni yasawa kwako? Je, waoneleaje kuhusu Dini isiyokuwa na kuhukumika, isiyo weka mahitaji au vikwazo, na ambayo haijafungwa au kuzingirwa na usumbufu mwingi wa vihitajikavyo na visivyo hitajika kufanywa? Iko nje kule, kama jinsi nilivyo elezea,lakini je, Dini ni kitu cha kuchagua kama ladha ya ice cream inayokupendeza?
Kunazo sauti nyingi zinazo shindania usikivu wetu, sasa kwa nini mtu afikirie kuhusu Yesu huko juu, sema Muhammad au Confucius (Mwana filosofia Fulani wa china), Buddha, au Charles Taze Russell, au Joseph Smith? Kwani hata hivyo si njia zote zinaelekea Mbinguni? Kwani si Dini zote ziko sawa? Ukweli ni kwamba Dini zote hazielekei Mbinguni kama jinsi ambavyo njia zote hazielekei Indiana.
Yesu pekee huzungumza kwa mamlaka ya Mungu kwasababu Yesu peke yake alishinda mauti. Muhammad,Confucius (Mwana filosofia Fulani wa china), na wengineo wanaendelea kubadilika kuwa mavumbi makaburini mwao mpaka leo hii, lakini Yesu, kwa nguvu zake, alitoka kaburini siku tatu baada ya kufa juu ya msalaba wa warumi uliojaa dhiki. Mtu yeyote mwenye uwezo juu ya mauti, ywastahili usikivu wetu. Mtu yeyote mwenye uwezo juu ya Mauti astahili kusikizwa.
Ushahidi unao simamia kufufuka kwa Yesu Kristo ni wa ushindi mkuu na haupingiki. Mwanzo, palikuwa na mashahidi zaidi ya mia tano waliokuwa wamefufuka kwa Kristo! Hao ni mashahidi wengi waliojionea kwa macho. Sauti mia tano haziwezi kupuuziwa. Pia kunalo jambo la kaburi lililokuwa tupu; maadui zake Yesu wangelikuwa wamesimamisha kwa njia ya rahisi habari zote za ufufuo kwa kuonyesha mwili wake, mwili ulio oza, lakini hawakuwa na mwili wowote wa kuonyesha! Kaburi lilikuwa tupu! Je, pengine mitume walikuwa wameuiba mwili? Ni vigumu. Kwa kuzuia uvumi huu usiokuwa wa kweli,kaburi lake Yesu lilikuwa limelindwa vilivyo na Askari waliokuwa wamejihami. Ukichunguza utaona marafiki wake wa karibu walikuwa wametoroka kwa uoga wa kukamatwa kwake na kusulubishwa, haingelikuwa rahisi kwa wavuvi waliokuwa wamevunjika moyo na kutishika, kupambana ana kwa ana na askari walio funzwa,na wenye ujuzi. Ukweli wa mambo nikwamba ufufuo wa Yesu hauwezi kubatilishwa!
Tena, yeyote aliye na mamlaka juu ya mauti astahili kusikilizwa.Yesu alithibitisha nguvu zake juu ya mauti, kwahivyo, twahitaji kusikia kile asemacho. Yesu asema ndiye njia ya pekee ya uzimani (Yohana 14:6). Yeye si njia tu; Yeye si mmoja kati ya njia nyingi, lakini Yesu ndiye njia.
Na Yesu huyu asema hivi, “Njoni kwangu,ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha’’ (Mathayo 11:28). Huu ni Ulimwengu mzito na maisha ni magumu. Wengi wetu tumefanyiwa madhambi, tumejeruhiwa, na tumetishika kivita. Ni kweli? Sasa, unataka nini? Uregesho ama dini tu? Mwokozi aishiye au Mmoja kati ya “Mitume’’ wengi waliokufa? Uhusiano wa maana au Kafara za utupu? Yesu si chaguo tu, Yeye ndiye chaguo!
Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta msamaha (Matendo 10:43). Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta uhusiano wa maana na Mungu (Yohana 10:10). Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta uzima wa milele Mbinguni (Yohana 3:16). Weka imani yako kwa Yesu kama Mwokozi wako-hutajilaumu! Mwamini yeye kwa msamaha wa dhambi zako-hutaaibika.
Kama ungelitaka kuwa na Uhusiano wa sawa na Mungu,hapa kunao mfano wa Maombi. Kumbuka yakwamba kwa kuomba Ombi hili au Ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyostahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa Neema yako ya ajabu na kwa msamaha-karama ya uzima wa milele! Amina!’’

Kipengele: Habari mpya, Mafundisho
0 Maoni