Je! Mungu Anao Ujumbe Wa Pekee Kwa siku zetu?
Ndiyo!
Ujumbe huo wa aina tatu unaonekana katika Ufunuo 14:6-16. kutangazwa
kwa ujumbe huo uliotolewa na malaika hao watatu kunafikia kilele chake
wakati ule wa kuja mara ya pili kwa Kristo (fungu la 14-16).
Ujumbe
wa Malaika wa Kwanza.
"Kisha nikamwona malaika mwingine, akiruka juu ya anga akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu, aitangaze kwa watu waishio duniani, kwa mataifa yote, makabila yote na watu wa lugha zote na rangi zote. Naye akasema kwa sauti kubwa, "Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi, bahari na chemchemi za maji" - (Ufunuo 14:6,7).
Ingawa
Maandiko yanaonyesha picha ya kuvutia ya ujumbe huo wa aina tatu kwa
njia ya mfano wa hao malaika watatu, watu wa Mungu ndio wajumbe hasa
wautangazao kwa ulimwengu mzima. Hawahubiri injili mpya, bali "injili
ya milele" kwa ulimwengu mzima- yaani, kwa kila taifa na kabila
na lugha na jamaa. "Injili ya milele" ya Kristo ni ujumbe
ule ule wa wokovu ambao watu katika kipindi kile cha Agano la kale waliupokea
" kwa imani" (Waebrania 3:16-19; 4:2; 11:1-40); ni mafundisho
yale yale aliyoyatangaza Yesu mwenyewe; ni injili ile ile iliyounguruma
katika karne zile zote za kipindi cha Kikristo.
Injili
hiyo rahisi, iokoayo, ya Yesu Kristo ilikuwa karibu imetoweka kabisa
katika Kanisa kwa zaidi ya miaka elfu moja katika kipindi cha zama za
giza (Dark Ages), lakini matengenezo ya Kanisa (Reformation) yaliifufua,
na watu wa Mungu wanaihubiri ulimwenguni kote leo. Malaika wa kwanza
anatangaza ujumbe wa injili iyo hiyo, lakini inahubiri katika mwelekeo
mpya - yaani, wa ulimwengu mzima - kwa ajili ya watu wanaoishi kabla
tu ya kuja Yesu mara ya pili.
Wale
wanaoupokea ujumbe huu wanajikuta wanaitwa ku "mch[a] Mungu na
kumtukuza [kuakisi tabia yake]." Wanauonyesha ulimwengu tabia ya
Mungu ya upendo, sio tu kwa maneno yao, bali pia kwa maisha yao yenye
ushuhuda wenye nguvu. Wanatoa ufunuo wa kusisimua wa kile Mungu awezacho
kufanya kupitia kwa watu waliojazwa na Roho wa Kristo.
Hivi
ni lini utakapotangazwa huo ujumbe wa malaika hao watatu katika ulimwengu
mzima? Wakati saa ya "hukumu yake [Mungu] imekuja." Mwongozo
13 unaeleza kwamba Yesu alianza kazi ya hukumu inayotangulia kabla ya
kuja kwake katika mwaka ule ule, yaani, 1844, Yesu aliwavutia watu ulimwenguni
kote kuanza kuhubiri ujumbe huo wa Ufunuo 14.
Ujumbe
huo unatuagiza sisi ku"msujudi[a] yeye aliyezifanya mbingu, [na]
nchi" [Ufunuo 14:7]. Mungu anatutaka sisi ku "ikumbuk[a] siku
ya Sabato [t]uitakase" kwa sababu "kwa siku sita Bwana alifanya
mbingu na nchi" (Kutoka 20:8-11). Katika mwaka ule wa 1844 Darwin
alipokuwa anaitoa nadharia yake ya evalusheni [kutokea vyenyewe tu vitu
vyote], Mungu alikuwa anawaita watu wake kurudi na kumsujudia yeye kama
Muumbaji wao. Wakati ule ule hasa, wale waliokuwa wakiuhubiri ujumbe
huo wa malaika watatu waliigundua Sabato ya siku ya saba ya neno la
Mungu, nao wakaanza kuitunza kwa kumheshimnu Muumba wa Mbingu na Nchi.
(2)
Ujumbe wa malaika wa pili.
"Malaika wa pili akafuata, akasema, 'Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu, uliowafanya mataifa yote kunywa mvinyo wa uasherati wake unaowafanya kuwa vichaa.!! - ufunuo 14:8.
Malaika
wa pili anaonya anasema, "Umeanguka Babeli Mkuu." Ufunuo 17
unaonyesha picha ya "Babeli" ya kiroho - yaani, Ukristo ulioasi
- kama mwanamke kahaba (fungu la 5). Anasema akiwa tofauti na mwanamke
safi wa Ufunuo 12 anayeliwakilisha kanisa la kweli la Kikristo. Mwanamke
anayewakilisha Babeli ni mwanamke aliyeanguka [aliyeasi] ambaye aliwafanya
"mataifa yote kunywa mvinyo wa uasherati wake unaowafanya kuwa
vichaa." Mvinyo wa mafundisho ya uongo umeenea kote katika mfumo
potofu wa Ukristo. Ujumbe huo wa malaika wa pili unawaita watu wa Mungu
kuyapinga mafundisho hayo ya uongo ya Ukristo huo ulioasi.
Babeli
unawakilisha mseto wa mifumo mingi ya Ukristo ulioasi. Ni wa hatari
mno kwa sababu unaipotosha picha ya Mungu na kuifanya kama vikaragosi
[sanamu za kuchekesha]: yaani, unamfanya Mungu kuwa ni mlipiza kisasi
na mwenye madai mengi, unamfanya Mungu kama babu yetu mwenye upendo
ambaye ni mwema mno kuweza kumsumbua mtu awaye yote juu ya dhambi zake.
Kanisa lenye afya litatoa picha yenye uwiano mzuri wa sifa zote za Mungu,
kisha litaonyesha jinsi haki na rehema yake inavyofungamana na kweli
isemayo kwamba Mungu ni upendo.
Mungu
anawaita watu wake anasema "tokeni" Babeli (Ufunuo 18:4),
anataka wayakatae mafundisho yale yasiyotoka katika Biblia, kisha wayafuate
mafundisho ya Kristo.
(3)
Ujumbe wa malaika wa tatu
"Na malaika wa tatu aliwafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, Yeyote anayemwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake juu ya paji la uso wake au juu ya mkono wake, yeye mwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu ambayo imemininwa katika kikombe cha ghadhabu yake bila kuchanganywa na maji. Mtu huyo atateseka ndani ya moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele ya Mwanakondoo. Moshi wa moto unaowatesa hupanda juu milele na milele. Watu hao waliomwabudu huyo mnyama na sanamu yake na kutiwa alama ya jina lake, hawatakuwa na nafuu yoyote usiku na mchana. Hivyo lazima watakatifu, yaani watu wanaotii amri ya Mungu na kumwamini Yesu, wawe na uvumilivu" - (Ufunuo 14:9-12).
Ujumbe
wa malaika wa tatu unaugawa ulimwengu wote katika makundi mawili. Upande
mmoja wanasimama Wakristo waasi [ yaani, wasiofuata mafundisho ya Biblia]
ambao hu "msujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea alama
yake katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake." Upande ule
mwingine wanasimama wale wanaoikataa mamlaka ya mnyama, yaani. Wale
"watakatifu wanaozitii amri [kumi] za Mungu na kuendelea kuwa waaminifu
kwa Yesu."
Zingatia
tofauti iliyopo kati ya makundi hayo mawili yanayopingana. Wale wanaoipokea
alama ya mnyama ni waabudu wanaoyalegeza masharti ya imani ambao wanafuata
mawazo yaliyotungwa na wanadamu yaonekanayo kama yanafaa pamoja na kuzifuata
desturi zao. "Watakatifu wanatabia hizi zinazowatambulisha: "uvumilivu"
utii kwa "Amri za Mungu" kisha "wanaendelea kuwa waaminifu
kwa Yesu."
Baada
ya ujumbe huo wa aina tatu kutangazwa ulimwenguni kote, Yesu atakuja
ku "vun[a] wale waliookolewa:
"Kisha, nikatazama, na kumbe palikuwapo wingu jeupe hapo. Na juu ya wingu hilo alikuwako aliye kama Mwana wa Mtu. Alikuwa amevaa taji ya dhahabu kichwani, na kushika mundu mkononi mwake. Kisha malaika mwingine akatoka hekaluni, na kwa sauti kubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu, "Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameivaa". Basi, yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu akautupa mundu wake duniani, na mavuno ya dunia yakavunwa" - (Ufunuo 14:14-16).
"Kisha, nikatazama, na kumbe palikuwapo wingu jeupe hapo. Na juu ya wingu hilo alikuwako aliye kama Mwana wa Mtu. Alikuwa amevaa taji ya dhahabu kichwani, na kushika mundu mkononi mwake. Kisha malaika mwingine akatoka hekaluni, na kwa sauti kubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu, "Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameivaa". Basi, yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu akautupa mundu wake duniani, na mavuno ya dunia yakavunwa" - (Ufunuo 14:14-16).
Kipengele: Habari mpya, Mafundisho, Tuisome Biblia, Ujumbe wa leo
0 Maoni