Ni hatua gani kuelekea wokovu?
Imani katika Yesu kama mwokozi ndio “hatua” pekee ya wokovu. Ujumbe wa Biblia uu wazi. Wote tumetenda dhambi kinyume na Mungu (Warumi 3:23). Kwa sababu ya dhambi zetu, tunastahili kutenganishwa na Mungu milele (Warumi 6:23). Kwa sababu ya upendo wake kwetu (Yohana 3:16), Mungu aliuchukua umbo la mwanadamu na akafa kwa ajili yetu, huku akichukua adhabu ambayo tulistahili (Warumi 5:8; 2Wakorintho 5:21). Mungu anaahidi msamaha wa dhambi na uzima wa milele mbinguni kwa wote wampokeao, kwa neema kupitia kwa imani katika Yesu Kristo kwa mwokozi (Yohana 1:12; 3:16; 5:24; Matendo 16:31).
Wokovu sio juu ya hatua fulani ambazo ni lazima tuzifuate ile tupate wokovu. Naam, Wakristo lazima wabatizwe. Naam, Wakristo lazima wamkiri hadharani Kristo ni mwokozi. Naam Wakristo lazima wageuke kutoka dhambi. Naam, Wakristo lazima wayatoe maisha yao kwa kumtii Mungu. Ingawa, hizi sio hatua za wokovu. Ni matokeo ya wokovu. Kwa sababu ya dhambi zetu, kwa njia yoyote hatuwezi jipatia wokovu. Tunaweza fuata hatua 1000, na hazitatosha. Ndio sababu Yesu akafa kwa ajili yetu. Kamwe hatuna uwezo wa kulipia dhambi zetu kwa Mungu kama deni ili tujitakaze kutoka dhambi. Ni mungu pekee angekamilisha wokovu, na kwa hivyo alifanya. Mungu mwenyewe alikamilisha “hatua” na papo hapo akautoa wokovu kwa ye yote atakayeupokea kutoka kwake.
Wokovu na msamaha wa dhambi sio mambo na hatua. Ni kumpokea Kristo kama mwokozi na kutambua ya kwamba amekwisha fanya kazi yote kwa niapa yetu. Mungu anahitaji hatua moja kutoka kwetu-kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi na kumwamini Yeye pekee kama njia ya wokovu. Hiyo ndio yatofautisha imani ya Kikristo kutoka kwa dini zote za ulimwengu, ambazo kila moja iko na orodha ya hatua ambazo ni lazima zifuatwe ili wokovu upatikane. Imani ya Kikristo yatambua ya kwamba Mungu amekwisha kamilisha hatua, na anatuita tumpokee kwa imani.
Kipengele: Habari mpya, Ujumbe wa leo


0 Maoni